Wednesday, October 24, 2012

Ndege ya Jeshi yaanguka na kuua mwanajeshi

Aina mojawapo ya ndege za kijeshi
 Ndege ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) imeanguka kuaa mwanajeshi mmoja na mwingine kujeruhiwa baada ya ndege hiyo ilikukuwa kwenye mafunzo kupoteza mwelekeo na kuanguka katika eneo la Ukonga jijini Dar es Salaam jana.

Msemaji wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania Kanali Kapambala Mgawe, alisema kuwa ndege hiyo ilikuwa kwenye harakati za kuruka ilipoteza mwelekeo.

Alisema wakati ndege hiyo ikijiandaa kuruka ikiwa na maofisa wa mafunzo wawili, ilipoteza mwelekeo na kuserereka na kuelekea ndani kwenye hanga kitendo kilichowafanya waamue kujinusuru maisha yao.

“Ndani ya hanga hilo kulikuwa na ndege nyingine mbili, lakini hata hivyo tunashukuru hakuna madhara yaliyotokea, kila kitu kiko salama,” alisema Kanali Mgawe.

Alisema wanajeshi hao, kila mmoja aliamua kuchumpa kwa mwamvuli ambapo Kapteni Magushi alianguka juu ya paa la jengo lililokuwa karibu na eneo hilo ndipo alipopoteza maisha.

Alimtaja mwanajeshi aliyenusurika katika tukio hilo, kuwa ni Kapteni Kwidika, ambaye amekimbizwa katika hospitali ya kijeshi Lugalo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kupatiwa matibabu.
Wanajeshi hao walikuwa katika shughuli zao za mafunzo ya kawaida

No comments: